VIDEO Queen asiyeishiwa vituko, Gift Stanford
‘Gigy Money’ amethibitisha kuwa yupo mbioni kumpiga kibuti bwana’ke mwarabu
endapo ataendelea kuwa bahili, kwani kwake yeye hakuna mapenzi isipokuwa
anachojali ni hela tu.

“Siku hizi hakuna mapenzi ya kugandana, mapenzi ni hela, mimi mwenyewe sina hela halafu nikampende mwanaume kapuku tutaendeshaje maisha sasa? Huwa sifanyi biashara hiyo, kikubwa kwangu nampenda mwanaume mwenye mkwanja, mwarabu anazo na mwanzoni alikuwa akinipa za kutosha, lakini sasa naona amekuwa bahili, namuacha,” alisema Gigy Money.
Chapisha Maoni
Zingatia: Mwanachama wa blogu hii tu ndiye anayeweza kuchapisha maoni.